Karibu Sabbath Light Ministry
<a

Mahubiri ya Krismasi ya mwaka 2017 yalikuwa kisiasa zaidi.

Katika picha ni Padri akiongoza ibada mjini Dusseldorf siku ya Krismasi. Angalia vidole vitatu karibu na Biblia, anaonyesha salamu ya kipagani inayoitwa Trident.Picha kutoka DW.

Katika baadhi ya habari zifuatazo, ni uthibitisho kwamba Krismasi ya mwaka 2017 ilikuwa ni mahubiri ya siasa kwa kiasi kikubwa kuliko mahubiri ya Injili.


Mhariri wa gazeti ayatuhumu makanisa ya Ujerumani.

“Mhariri mkuu wa gazeti la Die Welt, mojawapo ya magazeti yanayoongoza nchini Ujerumani na lenye mtazamo wa kihafidhina, amechochea mjadala katika mitandao ya kijamii wakati wa Krismasi baada ya kulalamika kwamba mahubiri yalikuwa ya upendeleo kwa mirengo ya kushoto katika misa ya usiku ya Krismasi. . . . Kauli yake ilikuja siku chache baada ya kiongozi wa chama siasa za mrengo mkali wa kulia cha AfD, Alice Wiedel kutoa malalamiko sawa kwa jarida la Focus akisema kwamba makanisa yameingiliwa na siasa. . . . Msemaji wa shirika la kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani EKD aliyatupilia mbali madai hayo ya Poschardt. Aliiambia DW kwa njia ya barua pepe kuwa “taswira hiyo ya kupotoshwa haionyeshi ukweli wa maelfu ya mahubiri ya Krismasi kote Ujerumani. Haikuelewa haki ya kiroho ya kauli ya kanisa juu a masuala ya siasa. Mtu aliye mwaminifu wakati mwingine ni lazima awe na siasa.” —(DW 28.12.2017, Mhariri Daniel Gakuba).


Polepole azungumzia viongozi wa dini kuhubiri siasa
Disemba 29, 2017

“Jana [28-12-17] Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, alitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.” —(Zanzibari 24, Disemba 29, 2017).

Kama ulisikiliza au ulitazama kwa makini maadhimisho ya Krismasi yaliyofanyika mwaka jana 24/12/2017 usiku katika mkesha, nadhani unajua kwamba mahubiri ya Krismasi kwa kiasi kikubwa yalilenga siasa zaidi kuliko Yesu Kristo.


Kunayo mipaka kati ya dini na siasa Tanzania?
Januari 3, 2018

Mwaka 2018 hatimaye umeanza. Wengi wamekuwa wakiusubiri kwa hamu wakidhani kwamba, huenda kuanza kwa mwaka mpya kunaweza kuleta mambo mapya. . .Nchini Tanzania hali ilikuwa tofauti kidogo. Viongozi wa dini nchini humo, kwa pamoja waliamua kutumia sikukuu ya Krismasi na ile ya Mwaka Mpya, kuhutubia amani lakini zaidi kuinyooshea kidole serikali kwa maana ya kuikosoa katika baadhi ya mambo. Aliyefungua ukurasa huo si mwengine, bali ni askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe ambae amenukuliwa akiitaka serikali itoe fursa kwa vyamba vya upinzani kutekeleza wajibu wake. . . Hata hivyo, kauli za viongozi hawa wa dini kwa serikali haikupokewa vizuri.

Serikali kuwaonya viongozi wa kidini

Serikali ya Tanzania imewatahadharisha viongozi hao wa dini kwa kuwa wanaingilia siasa. Hivyo kuwataka wakae mbali kabisa masuala ya kisiasa. Kauli hii ya serikali inaonekana kuzua mjadala mkali nchini, huku baadhi wakihoji ni ipi mipaka ya dini na siasa? Au ni wapi au ni wakati gani ambapo viongozi wa dini wanaruhusiwa kuzungumzia siasa na ni wakati gani ambapo hawaruhusiwi? . . .

Ni mara ya kwanza?

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini kuibuka na kuanza kuinyooshea vidole serikali iliyopo madarakani. Hayo yametokea katika awamu zote, ikiwemo serikali ya awamu ya nne ambayo ndio imetoka madarakani. . . Na hii pia sio mara ya kwanza kwa mjadala wa viongozi wa dini kulaumiwa kwa misingi ya kuchanganya dini na siasa kuibuka. . .

Siasa katika mahubiri

Pierre Whalon, ambaye ni askofu wa mkusanyiko wa makanisa katika nchi za Ulaya anasema, kwa mara kadhaa amekuwa akifuatwa na watu na kuambiwa aache kuingiza siasa katika mahubiri yake. Hata hivyo, anasema, muhimu ifahamike katika historia ya binadamu kwamba siasa na dini ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutenganishwa. “Kwa maana hiyo, haiwezekani kutenganisha dini na siasa, na yeyote anayejaribu kufanya hivyo, aidha anadanganya au hajafikiria vizuri,” anasema mchungaji huyo katika moja ya makala zake yenye kichwa, ‘Religion and Politics Are Inseparable: Get Over.’ (Dini na Siasa haziwezi Kutenganishwa: Kubali hayo). Suala la dini na siasa ni la muda mrefu sana, na halijazua mjadala katika nchi za Kiafrika pekee, bali hata katika zilizoendelea ambazo wengi wanaamini kwamba ndipo kwenye ukomavu wa demokrasia.

Swali hili pia limejitokeza katika kitabu kiitwacho,Religious Convictions and Political Choice(Itikadi za Kidini na Uamuzi wa Kisiasa), kilichoandikwa na Kent Greenawalt. Swali hilo hilo, limejibiwa katika kitabu cha zaidi ya kurasa 200, lakini mwisho wa siku, imeonyesha dhahiri kwamba, siasa na dini vina ukaribu mkubwa sana, na imani ya dini siku zote ina ushawishi mkubwa sana hata kwa wanasiasa wenyewe.” –(BBC Swahili 3 Januari 2018).


Advertisements