Imani za zamani 1844-1900 hazibadiliki

Hatua za kiadventista tangu mwaka 1844, zilanzishwa katika msingi mgumu na wa milele usiweza kubadilishwa mpaka mwisho wa dunia, Ellen White mpaka kufa kwake bado alionya imani yetu isibadilishwe. Ingawa kuna watu wanaodai kuna “ukweli endelevu”, lakini huu ni uongo mkubwa, ukweli mpya hauwezi kuhitilafiana na ukweli wa zamani. Ellen White alionyesha wazi kwamba mafundisho yetu yalidhihirishwa kwa Roho Mtakatifu kama ukweli, na kuyabadilisha ni sawa na kusema Roho Mtakatifu alikosea.

“Ni ushawishi gani lakini ule wa mwongo unaoweza kuwaongoza watu katika hatua hii ya historia yetu kufanya kazi kwa njia ya uongo yenye nguvu ili kuangusha chini misingi ya imani yetu—misingi ambayo iliwekwa katika mwanzo wa kazi yetu kwa kujifunza Neno kwa maombi na kwa ufunuo. Juu ya misingi hii tumekuwa tukijenga kwa miaka hamsini iliyopita. Je msingi mpya utajengwa na watu ambao Mungu hajawapa uzoefu maalum alioutoa kwa watu ambao aliwaweka kuaanzisha misingi ya imani yetu? Watu ambao wanajitahidi kujenga msingi huu wa uongo wanaweza kudhani kwamba wamepata njia mpya, na kwamba wanaweza kuweka msingi mgumu kuliko ule uliowekwa. Lakini huu ni uongo mkubwa. Msingi mwingine hakuna awezaye kuuweka isipokuwa ule ambao umekwishakuwekwa.” —(Ellen G. White, Letter (Lt) 232, 1903, par. 45)

Ellen White aliandika haya mwaka 1903, na anasema msingi uliokuwa umejengwa kwa miaka hamsini iliyopita haubadiliki kabisa. Je unaamini kwamba Mungu aliongea kupitia Ellen White?

“Neno la Bwana limezilinda hatua zetu tangu kupita kwa wakati wa mwaka 1844. Tumeyatafuta Maandiko; tumejenga kwa ugumu; na hatupaswi kubomoa misingi yetu na kuingiza mbao mpya.” —(Ellen G. White, Letter 24, 1907, p. 3, par. 7); pia Manuscript Releases, vol. 1, p. 54.1; na vol. 2, p. 186.1))

“Hebu na asiwepo mtu wa kutafuta kuangusha chini misingi ya imani yetu—misingi ambayo iliwekwa katika mwanzo wa kazi yetu kwa kujifunza Neno kwa maombi na kwa ufunuo. Juu ya misingi hii tumekuwa tukijenga kwa miaka hamsini iliyopita. Je msingi mpya utajengwa na watu ambao Mungu hajawapa uzoefu maalum alioutoa kwa watu ambao aliwaweka kuaanzisha misingi ya imani yetu? Watu ambao wanajitahidi kujenga msingi huu wa uongo wanaweza kudhani kwamba wamepata njia mpya, na kwamba wanaweza kuweka msingi mgumu kuliko ule uliowekwa. Lakini huu ni uongo mkubwa. Msingi mwingine hakuna awezaye kuuweka isipokuwa ule ambao umekwishakuwekwa.” —(Ellen G. White, The Review and Herald (RH) March 3, 1904, par. 13); pia Testimony Treasures, vol. 3, p. 274.2; Testimonies for the Church, vol. 8, p. 297.1; na Gospel Workers 1915, p. 307.1)))

Kubadilisha misingi ya imani ingemaanisha tumeasi kutoka kwenye ukweli.

“Wengi wa watu wetu hawajui ni thabiti kwa kiasi gani msingi wa imani yetu umewekwa. Mume wangu, Mzee Bates, Baba pierce, Mzee [Hiram] Edson, na wengine ambao ni wenye bidii, waadilifu, na wa kweli, walikuwa miongoni mwa wale ambao baada ya kupita muda wa mwaka 1844, waliutafuta ukweli kama hazina iliyofichika. Nilikutana nao, na tulijifunza na kuomba kwa bidii. Mara nyingi tulibaki pamoja mpaka usiku ulipoenda, na wakati mwingine kupitia usiku wote, tukisali kwa ajili ya nuru na kujifunza Neno. Tena na tena ndugu hawa walikutana pamoja kujifunza Biblia, ili kwamba waweze kuijua maana yake na kujiandaa kuihubiri kwa nguvu. Wakati walipofika katika hatua ya kujifunza kwao ambapo walisema, “Hatuwezi kufanya zaidi” Roho wa Mungu angelikuja juu yangu. Nikachukuliwa katika maono, na ufafanuzi ulio wazi wa fungu tulilokuwa tukijifunza ulitolewa kwangu, kwa mafundisho kama jinsi gani tulipaswa kufanya kazi na kufundisha inavyotakiwa. Hivyo nuru ilitolewa ambayo ilitusaidia kuyaelewa Maandiko kumhusu Kristo, kazi yake, na Ukuhani wake. Mstari wa ukweli unaongezeka kutoka wakati ule hadi wakati tutakapouingia mji wa Mungu, iliwekwa wazi kwangu, na nilitoa kwa wengine maagizo ambayo Bwana amenipa…

“Ni ushawishi gani ambao utawaoongoza watu katika hatua hii ya historia yetu kufanya kazi katika njia ya udanganyifu wenye uwezo ili kubomoa msingi wa imani yetu-msingi ambao uliwekwa mwanzoni mwa imani yetu kwa kujifunza neno kwa maombi na ufunuo? Juu ya msingi huu tumekuwa tukijenga kwa miaka hamsini iliyopita.” —(Ellen G. White, Selected Messages Book 1 (1SM), pp. 206.4, 207.3); pia Christ in His Sanctuary, p. 6.2; na Special Testimonies Series B02, pp. 56.4, 58.1)))

Baadhi hudai kwamba Ellen White alibadirisha imani yake kuhusu Mungu, lakini huu ni uongo mkubwa, Ellen White mwenyewe alisema wazi kwamba:

“Ambacho nimekwishakukiadika ndicho Bwana alinitaka nikiandike. Sijaelekezwa kubadilisha kile ambacho nimekituma nje. Nasimama imara katika imani ya Kiadventista; kwa maana nimeonywa kuhusu falsafa za uongo ambazo zitatafuta kuingia miongoni mwetu kama watu. Maandiko yanasema, ‘Baadhi ya watu watajitenga na imani na kuziandamia roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.’ Ninawakilisha mbele ya watu wetu hatari ya kuongozwa kwenye kosa kama walivyoongozwa malaika katika mabaraza ya mbinguni. Msitari wa ukweli ulionyooka ambao uliwakilishwa kwangu wakati nikiwa msichana bado kwa wazi unawakilishwa kwangu sasa.” -(Ellen G. White, The Review and Herald January 26, 1905, paragraph 19)

Ellen White aliandika haya 1905 na anasema ukweli alioonyeshwa akiwa msichana mdogo, ndio ukweli anaoonyeshwa sasa. Hivyo Ellen White hakubadili imani yake tangu awali.

“Ushahidi uliotolewa katika uzoefu wetu wa mwanzo una nguvu zile zile ulizokuwa nazo. Ukweli ni ule ule kama ambavyo umekuwa daima, na hakuna pini au mhimili unaoweza kutoka kwenye jengo la ukweli. Ambao ulitafutwa katika Neno mwaka 1844, 1845, 1846 unabaki kama ukweli katika kila sehemu.” —(Ellen G. White, Letter 38, 1906, par. 3); pia Manuscript Releases, vol. 1 [Nos. 19-96], p. 52.1))

“Kweli tulizopewa baada ya kupita wakati wa mwaka 1844 ni za hakika kabisa na zisizobadilika kama Bwana alivyozitoa kwetu katika jibu kwa maombi yetu ya dhati. Maono ambayo Bwana amenipa ni ya ajabu sana kwamba tunajua kile ambacho kinakubalika kuwa ni ukweli. Hii ilidhihirishwa na Roho Mtakatifu. Nuru, nuru za thamani kutoka kwa Mungu, zilianzisha hatua kuu za imani yetu kama tunavyozishikilia leo.” –(Ellen G. White, Letter 50, 1906, p 1, 2); pia Manuscript Release No. 760, p. 22.1, Manuscript Releases, vol. 8, pp. 245, 319; na vol. 1, p. 53.2))

Angalia katika maelezo yafuatayo Ellen White anasema kubadilishwa kwa kweli za mwanzo kutaleta mafundisho ya uongo kuhusu nafsi ya Mungu na nafsi ya Kristo, na hivyo kuharibu fundisho la patakatifu pa mbinguni.

“Wale ambao hutafuta kuondoa minala ya zamani hawafanyi kwa uaminifu; hawakumbuki ni kwa jinsi gani walizipokea na kuzisikia. Wale wanaojaribu kuleta nadharia ambazo zitaondoa mihimili ya imani yetu kuhusu Patakatifu au kuhusu Nafsi ya Mungu au ya Kristo, wanafanya kazi kama vipofu. Wanataka kuleta mashaka na kuwafanya watu wa Mungu wachukuliwe na mkondo wa maji bila nanga.” —(Ellen G. White, Ye Shall Receive Power (YRP), p. 235, par.4); pia Manuscript Release No. 760, p. 9.5; Ms 62, 1905, par. 14; na The Integrity of the Sanctuary Truth, p. 9.5))

“Siku zijazo uongo wa kila aina utatokea, na tunahitaji aridhi ngumu kwa ajili ya miguu yetu. Tunahitaji mihimili migumu kwa ajili ya jengo. Hata pini moja isiondolewe kutoka katika kile ambacho Bwana amekianzisha. Adui ataleta nadharia za uongo, kama vile fundisho la kwamba hakuna Patakatifu. Hii ni moja katika mawazo ambayo kwayo kutakuwa na kujitenga kutoka katika imani. Wapi tutapata usalama mpaka iwe katika kweli ambazo Bwana amekuwa akizitoa kwa miaka hamsini iliyopita?” –(Ellen G. White, The Review and Herald (RH), May 25, 1905, par. 27); pia Ye Shall Receive Power, p. 239.2; Our Father Cares, p. 327.4; Maranatha, p. 192.4; na Manuscript Release No. 760, p. 12.3)))

Ellen White anaelezea zaidi kwamba imani yetu haibadiliki kwa jinsi yoyote ile.

“Miaka hamsini iliyopita haijafifisha nukta moja au kanuni ya imani kama tulivyozipokea shuhuda kuu na za ajabu ambazo zilifanywa kuwa hakika kwetu katika mwaka 1844, baada ya kupita kwa wakati…Hakuna neno lililobadilika au lililokataliwa. Ambalo Roho Mtakatifu alilithibitisha kama ukweli baada ya kupita kwa wakati, wa hali yetu ya kuvunjika moyo, ni msingi mgumu wa ukweli.” —(Ellen G. White, Special Testimonies, Series B7 (SpTB07), p 58, par. 1); pia The Upward Look, p. 352.4; Letter 326, 1905.3; Manuscript 111, 1905.4; na The New York Indicator Feb. 7, 1906, par. 4))

“Kweli ambazo zimekuwa zikiimarishwa kwa kazi dhahiri ya Mungu ni za kusimama imara. Na asiwepo mtu wa kuthubutu kuondoa pini au jiwe la msingi kutoka kwenye jengo. Wale ambao hujaribu kudhofisha mihimili ya imani yetu wako miongoni mwa wale ambao Biblia inawasemea kwamba, Katika siku zijazo wengine watajitenga na imani, na kuziandamia roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.” —(Ellen G. White, Letter (Lt) 87, 1905, par. 8); pia Manuscript Releases, vol. 1, p. 55.2; vol. 7, p. 189.4; na Bible Training School March 1, 1915, par. 4))

“Ni ushawishi gani ambao utawaongoza watu katika hatua hii ya historia yetu kufanya kazi katika njia yenye nguvu ya udanganyifu ili kubomoa msingi wa imani yetu—msingi ambao uliwekwa katika mwanzo wa kazi yetu kwa kujifunza neno kwa maombi na ufunuo? Juu ya msingi huu tumekuwa tukijenga kwa miaka hamsini iliyopita. Je unashangaa kwamba wakati ninapoona mwanzo wa kazi ambayo ingeondoa baadhi ya mihimili ya imani yetu, nina kitu cha kusema? Ni lazima nitii amri ‘Kutana nayo'”… —(Ellen G. White, Selected Messages Book 1 (1SM), p. 207.3))

“Hatuna chochote cha kuhofia kwa ajili ya wakati ujao, isipokuwa kama tutasahau njia ambayo Bwana ametuongoza nayo, na mafundisho yake katika historia yetu iliyopita.” —(Ellen G. White, Life Sketches (LS), 196.2); pia Selected Messages Book 3, p. 162.3; Counsels for the Church, p. 359.4; Christian Experience and Teachings, p. 204.1; na Last Day Events, p. 72.1))

Je mafundisho yetu ya awali yamesahauliwa? Je ni hatari gani iliyopo sasa kwa watu wa Mungu?

“Na mara tu nafsi hizi zilizouamini uongo zilipojitenga kutoka kwenye minara ya imani ya zamani, waliiacha nanga yao iende, na walijirusha kwenye mawimbi ya bahari.” —(Ellen G. White, The Signs of the Times March 27, 1884, par. 2); pia Statements Relating to Geology and Earth Sciences, p. 8.1))

Hivyo kuiacha imani na kweli zetu za zamani ni sawa na kujirusha kwenye mawimbi ya maji; kwa maana kweli hizo ni meri, na kuziacha ni sawa na kuiacha meri, na hatutafika mbinguni ikiwa tumezidharau kweli hizo.

“Hivi juzijuzi nimesoma kuhusu boti adilifu ambayo ilikuwa inasafiri katika njia yake baharini, wakati wa usiku wa manane, kwa mgongano wa kutisha, iligonga kwenye mwamba; wasafiri waliamshwa kuona kwa hofu hali yao isiyo na matumaini, na pamoja na boti walizama wasiinuke tena. Mtu aliyekuwa anaendesha alikuwa amekosea nuru ya mnara wa ishara [beacon light], na mamia ya nafsi zilikuwa katika onyo la wakati huo lililoanzishwa milele.” —(Ellen G. White, Selected Messages Book 2 (2SM), p. 128, par. 3))

“Tumezurura mbali na minara ya zamani. Hebu na turudi. Kama Bwana ni Mungu, mtumikieni yeye; kama Baali mtumikieni yeye. Je utakuwa upande gani?” —(Ellen G. White, Testimony Treasures, vol. 2 (2TT), p. 32.1); pia Testimonies for the Church, vol. 5, p. 137.3)).

Je umezurura mbali na minara ya zamani? Kumbuka kweli za zamani ndiyo meri itakayotufikisha mbinguni salama, kuzikataa hizo ni sawa na kujirusha kwenye mawimbi ya maji na kupotea milele.

“Mko katika hatari ya kushindwa kushikilia imara imani iliyokabidiwa mara moja tu kwa watakatifu, hatari ya kuzama meri ya imani yenu…Tobo dogo sana litaizamisha meri.” —(Ellen G. White, Counsels on Health (CH), p. 519, par. 1); pia Testimonies for the Church, vol. 8, p. 158.1)

Sasa nini ambacho tunatakiwa kufanya ili kuepuka hatari hii? Ni kurudia kweli za zamani!

“Hatuwezi kukubali kudanganywa. Ni lazima tuwaongoze watu wetu kwenye minara ya zamani. Tunapaswa kupata nguvu na ujasiri kutoka juu, ili kwamba tuweze kutii amri niliyopewa ‘kutana nayo.’” —(Ellen G. White, Letter 249, 1903, par. 5); pia Manuscript Releases, vol. 7 [Nos. 419-525], p. 384.1))

“Kama sisi ni Wajumbe wa Bwana walioteuliwa, hatutainuka na mawazo na nadharia mpya ili kuhitilafiana na ujumbe ambao Mungu ameutoa kupitia watumwa wake tangu mwaka 1844. Katika wakati ule wengi walimtafuta Bwana kwa moyo na nafsi na sauti. Watu ambao Mungu aliwainua walikuwa watafutaji wa Maandiko wenye bidii. Na wale ambao leo hudai kuwa wana nuru, na ambao huhitilafiana na fundisho la wajumbe waliowekwa na Mungu, ambao walikuwa wakifanya kazi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, wale ambao wanaleta nadharia mpya, ambazo zinaondoa mihimili ya imani yetu, hawafanyi mapenzi ya Mungu, lakini wanaleta dhana za uongo za uvumbuzi wao wenyewe, ambazo, kama zikipokelewa, zitalikata kanisa mbali na gatini [mahali panapokaa meli] pa ukweli, na kuwafanya waelee majini, waelee majini, kwenda popote watakakopokea makosa yoyote yatakayoinuka.” —(Ellen G. White, Manuscript 75, 1905, par. 5); pia The Integrity of the Sanctuary Truth, p. 14.2))

“Kazi yetu ni kutoa sababu zenye nguvu za imani yetu, kwa sababu kuna watu ambao, kamwe hawajaimarishwa katika ukweli, wataleta uongo ambao utabomolea mbali gatini pa imani yetu, Mungu hatumi mtu akiwa na ujumbe ambao utaongoza nafsi kujitenga kutoka kwenye imani ambayo imekuwa ngome yetu. Tunapaswa kuthibitisha imani hii badala ya kubomoa msingi ambao juu yake inakaa.” —(Ellen G. White, Manuscript 75, 1905, par. 6); pia Manuscript Release No. 760, p. 14.3; na The Integrity of the Sanctuary Truth, p. 14.3))

Kweli za zamani lazima zirudiwe, vinginevyo watu hawatafika bandarini.

“Kutakuwa na kubadilika mioyo mara ya pili kwa baadhi ya viongozi wetu wa umoja wa tiba, na kukatiwa mbali kutoka katika watu ambao wanajaribu kuiongoza boti ya tiba kwenda bandarini, vinginevyo kamwe hawatafikia kituo cha kupumzika. Kristo anaita, Tokeni kati yao, na mkatengwe nao.” —(Ellen G. White, Manuscript 21, 1906, par. 17); pia Testimonies for the Church Containing Messages of Warning and Instruction to Seventh-day Adventists (SpTB07), p. 63.3)))

“Sasa ninatoa ujumbe alionipa Mungu, kuutoa kwa wote ambao hudai kuuamini ukweli, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” vinginevyo dhambi zao katika kufanyia haki makosa na kutunga uongo yataendelea kuwa ni maangamizo ya nafsi. Hatuwezi kukubali kuwa upande wa kosa. Hatuwezi kukubali kuufunika ukweli kwa matatizo ya kisayansi. Tuna hamu kwamba mabadiliko ya kuuamua yafanywe, na hakuna kutapatapa zaidi-Vizuizi viwekwe mbele ya miguu ya watu wa Mungu. Kila nafsi na ivae viatu vya injili. Kila nafsi na iombe na kufanya kazi, ili kuiweka miguu yao juu ya msingi alioweka Kristo kwa kuutoa uhai wake kwa ajili ya uhai wa ulimwengu.”. —(Ellen G. White, Manuscript (Ms) 21, 1906, par. 20); pia Testimonies for the Church Containing Messages of Warning and Instruction to Seventh- day Adventists (SpTB07), p 64.2))))

“Ninajua kutoka katika nuru ambayo Bwana amenipa kwamba lazima kutakuwa na uhuishaji wa jumbe ambazo zimetolewa katika nyakati zilizopita, kwa sababu watu watatafuta kuingiza nadharia mpya, na watajaribu kuthibitisha kwamba nadharia hizi ni za kimaandiko, wakati wako katika kosa, ambalo, kama likiruhusiwa, litadhoofisha imani katika kweli. Hatupaswi kukubali mawazo haya na kuyapitisha kama ukweli. Hapana, hapana; lazima tusitoke kwenye jukwaa la ukweli ambao tumekuwa tukianzisha.

“Siku zote kutakuwa na wale ambao wanatafuta kitu kipya, na ambo hupanua na kulifanyia bidii sana Neno la Mungu ili kulifanya liyaunge mkono mawazo yao na nadharia.Hebu ndugu zangu, na tuchukue vitu ambavyo Mungu ametupa, na ambavyo Roho wake ametufundisha ni kweli, na tuviamini, na kuziacha peke yake nadharia hizo ambazo Roho wake hajazifundisha.” —(Ellen G. White, The Upward Look (UL), p. 199, par. 6); pia Our Father Cares, p. 271.6; Manuscript 125, July 4, 1907.17; Manuscript Release No. 760, p. 31.2; na Sermons and Talks, vol. 1, p. 387.1))

Ukweli ulioimalishwa zamani ni wa milele.

“Waache Waasisi wautambulishe ukweli.—Wakati uwezo wa Mungu ukishuhudia kama kipi ni ukweli, ukweli huo unasimama milele. Hakuna mawazo, yaliyo kinyume na nuru aliyoitoa Mungu yanayopaswa kupokelewa. Watu watainua utafisiri wa Maandiko ambao kwao ni ukweli, lakini ambao sio ukweli. Ukweli kwa wakati huu, Mungu ameutoa kwetu kama msingi kwa ajili ya imani yetu. Yeye Mwenyewe ametufundisha kipi ni ukweli. Mtu atainuka, na bado mwingine naye atainuka, na nuru mpya ambayo inahitilafiana na nuru ambayo Mungu ameitoa chini ya udhihirisho wa Roho Wake Mtakatifu.

“Wachache tu bado wako hai ambao walipitia uzoefu uliopatikana katika uanzishwaji wa ukweli huu. Mungu kwa neema ameyatunza maisha yao kurudia na kurudia mpaka kufungwa kabisa kwa maisha yao, uzoefu ambao wameupitia kama vile alivyofanya Yohana mtume mpaka kufungwa kabisa kwa maisha yake. Na wachukua-viwango ambao wameangukia katika mauti, wanapaswa kuongea kupitia kuyachapisha maandiko yao. Nimeagizwa kwamba sauti zao zinapaswa kusikiwa. Wanapaswa kutoa ushuhuda wao wa kipi kinaunda ukweli wa wakati huu.

“Hatupaswi kupokea maneno ya wale ambao huja na ujumbe unaohitilafiana na hatua maalumu za imani yetu. Wanakusanya pamoja lundo la Maandiko, na kulirundika kama ushahidi kuzunguka nadharia zao wanazozitetea. Hili limekuwa likifanyika tena na tena wakati wa miaka hamsini iliyopita. Na wakati Maandiko ni neno la Mungu, na yanapaswa kuheshimiwa, matumizi yao, ikiwa matumizi kama hayo yanaondoa mhimili kutoka kwenye msingi ambao Mungu ameuizinisha kwa miaka hii hamsini, ni kosa kubwa. Yeye ambaye anafanya matumizi kama hayo hajui udhihirisho wa ajabu wa Roho Mtakatifu ambaye alitoa nguvu na msukumo katika jumbe zilizopita ambazo zimekuja kwa watu wa Mungu.” —(Ellen G. White, Preach the Word (PW), p. 5); pia Counsels to Writers and Editors, p. 31.2)))

“Baadhi ya wale ambao ni wapya wanaokuja katika imani na kudai kwamba wana nuru maalumu kutoka kwa Mungu katika kuhusu jumbe hizi; lakini nuru yao mpya huwaongoza kuweka mbali kweli zilizoanzishwa ambazo ni mihimili ya imani yetu. Wametafsiri vibaya na kutumia vibaya Maandiko. Wanaziweka vibaya jumbe za Ufunuo 14, na kuiweka pembeni kazi ambayo jumbe hizi zimeikamilisha. Hivyo wanakataa mipaka ambayo Mungu mwenyewe ameianzisha. Kwa sababu nuru yao mpya inawaongoza kubomoa jengo ambalo Bwana alilijenga, tunapaswa kujua kwamba Yeye hawaongozi.” —(Ellen G. White, 1888 Materials (1888), p. 804, par. 1); pia Manuscript 31, 1890, par. 7))

“Bwana amesema wazi kwamba historia iliyopita itasimuliwa kadri tunavyoingia katika kufanya kazi. Kila kweli ambayo ameitoa siku hizi za mwisho itatangazwa ulimwenguni. Kila mhimili ambao ameuanzisha utaongezwa nguvu. Hatuwezi sasa kuuacha msingi ambao Mungu ameuanzisha. Hatuwezi kuingia katika jumuiya yoyote mpya; kwa maana hii itamaanisha uasi kutoka katika kweli…Kuna hitaji sasa la kusimulia uzoefu wa watu ambao walifanya sehemu katika uanzishaji wa kazi yetu hapo mwanzo.” —(Ellen G. White, Manuscript (Ms) 129, 1905, par. 6); pia Manuscript Releases, vol. 1, p. 54.2; vol. 20, p. 151.1; Christ Triumphant, p. 367.6; Testimony Treasures, vol. 2, p. 363.2; Selected Messages Book 2, p. 390.1; na Notebook Leaflets, vol. 1, p. 51.7))

“Nimekuwa nikiagizwa kuwaonya watu wetu; kwa maana wengi wako katika hatari ya kupokea nadharia na uongo ambao unadhoofisha msingi wa mihimili ya imani.”—(Ellen G. White, Selected Messages Book 1 (1SM), p. 196, par. 4); pia Testimonies for the Church Containing Letters to Physicians and Ministers Instruction to Seventh-Day Adventists, p. 15.2; na Letter 263, 1904.13))

“…lazima kwa uthabiti tukatae kuvutwa mbali na jukwa la ukweli wa milele, ambao tangu 1844 umeshinda majaribu.” —(Ellen G. White, Selected Messages Book 1 (1SM), p. 199, par. 5); pia Special Testimonies, Series B7, p. 50.1; Manuscript Releases, vol. 1, p. 53.4; na Letter 277, 1904.17))

“Wachache wanaweza kutambua matokeo ya kukaribisha uongo unaotetewa na baadhi ya watu kwa sasa. Lakini Bwana ameinua pazia, na amenionyesha matokeo ambayo yatafuata. Nadharia za kiumizimu kuhusu nafsi ya Mungu, zikifuatwa kwa hitimisho lake la kimantiki, zitafagilia mbali uchumi mzima wa Kikristo. Wanaikisia kama kitu bure nuru ammbayo Kristo alikuja kutoka mbinguni kutmpa Yohana aitoe kwa watu wake. Wanafundisha kwamba matukio yaliyo mbele yetu kabisa si ya umuhimu wa kutosha kupewa kipaumbele maalum. Wanaufanya usio na faida ukweli wa asili ya mbinguni, na kuwaibia watu wa Mungu uzoefu wao wa nyuma, badala yake wanawapa sayansi ya uongo.”

“Katika maono ya usiku nilionyeshwa kwa wazi kwamba maono haya yamekuwa yakiangaliwa na baadhi kama kweli kuu ambazo zinapaswa kupelekwa na kufanywa maalum katika wakati uliopo. Nilionyeshwa Jukwaa, limekazwa kwa mbao ngumu—Kweli za Neno la Mungu. Mtu mmoja mkuu katika madaraka katika kazi ya kitabibu alikuwa anamuongoza mtu huyu na mtu yule kuregeza mbao zinazolisaidia Jukwaa hili. Kisha nikasikia sauti ikisema, ‘Wako wapi walinzi ambao walipaswa kusimama katika kuta za Sayuni? Je wamelala? Msingi huu ulijengwa na Bwana wa Kazi, na utahimili dhoruba na tufani, Je watamruhusu mtu huyu kuleta mafundisho ambayo yanakataa uzoefu wa wakati wa nyuma wa watu wa Mungu? Wakati umefika wa kuchukua kitendo kilichoamriwa.

“Adui wa roho amejaribu kuleta kile kinachodhaniwa kwamba ni uamsho mkuu ambao ungetokea kwa Waadventista Wasabato, na kwamba uamsho huu ungefuatana na kuacha mafundisho yaliyo mihimili ya imani yetu, na kujihusisha na kitendo cha kulipangilia upya Kanisa. Kama uamsho huu ungetokea, nini kingetendeka? Kanuni za ukweli ambazo Mungu katika hekima yake amelipatia Kanisa la Masalio zingeachwa. Dini yetu ingebadiliswa. Kanuni za lazima ambazo ndizo zimelitegemeza Kanisa katika kazi yake kwa miaka hamsini sasa zingehesabiwa kama makosa. Jumuiya mpya ingesimamishwa. Vitabu vya mpango mpya vingeandikwa. Mfumo wa falsafa za akili ya kidunia ungeletwa Kanisani. Waanzilishi wa mfumo huu wangeenda mijini, na kufanya kazi kubwa na ya ajabu. Sabato, kwa hakika, ingechukuliwa bila uzito, hali kadhalika na Mungu aliyeiumba. Hakuna ambacho kingeweza kusimama kinyume na mfumo mpya. Viongozi wangefundisha kwamba wema ni bora zaidi kuliko kosa, lakini Mungu akiwa ameondolewa, wangeweka mategemeo yao katika nguvu za mwanadamu, ambaye, bila Mungu, ni bure. Msingi wao ungejengwa kwenye mchanga, tufani na dhoruba ingetowesha jengo.

“Nani ana mamlaka ya kuanzisha mfumo kama huo? Tunazo Biblia zetu. Tunao uzoefu wa maisha, uliojaribiwa kwa utenda kazi wa Roho Mtakatifu. Tunao ukweli ambao hauruhusu mapatano na dunia. Je, hatutakataa kila kisichoendana na ukweli?” —(Ellen G. White, Selected Messages Book 1 (1SM), pp 203.4, 204.1-2 na 205.1); pia Special Testimonies Series B02, pp. 54-55))

“Tunachotaka sasa ni kuunda jumuiya upya. Tunataka kuanza kwenye msingi, na kujenga juu ya kanuni tofauti.” —(Ellen G. White, Last Day Events (LDE), p. 53.1); pia The General Conference Bulletin April 3, 1901, par. 25; vol. 4 April 3, 1901, p. 25.3; na 1888 Materials, p. 1745.3))

Sasa viongozi wamezibadilisha imani kinyume na maagizo ya Mungu kupitia dada White, na wanadai kwamba wamepata ukweli mpya, huu ni uongo mkubwa, ukweli mpya hauwezi kupingana na ukweli wa zamani. Angalia maelezo yafuatayo.

“Katika kila wakati kuna uongezekaji wa ukweli mpya, ujumbe wa Mungu kwa watu wa kizazi hicho. Ukweli wa zamani ni wa lazima; ukweli mpya sio wa kutofautiana na wa zamani, lakini wa kuutangaza wa zamani. Ni mpaka tu kama ukweli wa zamani unaeleweka ndipo tunaweza kuufahamu ukweli mpya.” —(Ellen G. White, The Signs of the Times June 20, 1906, par. 4); pia Christ’s Object Lessons, p. 127.4; na Lift Him Up, p. 306.4))

“Hakuna mstari wa ukweli ambao umewafanya watu wa Kiadventista wa siku ya saba jinsi walivyo, unaopaswa kudhoofishwa. Tuna minara ya zamani ya ukweli, uzoefu, na wajibu, na tunapaswa kusimama imara katika kutetea kanuni zetu katika mtazamo kamili wa dunia.” -(Ellen G. White, Australasian Union Conference Record January 1, 1901, par. 7)

Advertisements

Comments are closed.

%d bloggers like this: