Umoja wa watu wa Mungu

Je Ellen White alifundisha nini kuhusu umoja miongoni mwa watu wa Mungu? Kumbuka kuwa umoja ni wa muhimu sana kwa watu wote wanaomfuata Kristo, Yesu katika Yohana 17 aliomba kuwa watu wake wawe na umoja ili ulimwengu upate kujua ya kuwa Mungu amewatuma. Ellen White anafundisha kuwa umoja ni wa lazima kuwepo ili kazi ya Mungu iweze kufanyika na nguvu iwepo miongoni mwa watu. Lakini hata hivyo, umoja ni katika ukweli tu, na sio katika makosa, hatuwezi kuwa wamoja na wale wanaofundisha uongo. Kristo akiombea swala la umoja alisema “watakase katika kweli, neno lako ndiyo kweli”, kwamba wote wanaoiamini kweli ya Biblia ndio pekee wanaweza kuwa na umoja na si vinginevyo; na kama ikiwa vinginevyo ndipo Kristo anasema: “sikuja kuleta amani bali mafarakano”.

“Neno la Mungu likijifunzwa na kueleweka na kisha kulitii, nuru kamili huangazia ulimwengu, ukweli mpya ambao unapokelewa na kufanyiwa kazi, utatuunganisha na Kristo kwa kamba zilizo imara. Biblia na Biblia peke yake ndiyo kanuni yetu na ndicho kifungo kinachotuunganisha katika umoja, watu wote wanaonyenyekea mbele ya Neno hilo takatifu, wataishi katika umoja. Juhudi zetu hazipaswi kuongozwa na mitazamo yetu au mawazo yetu. Mwanadamu hukosea, lakini Neno la Mungu ndilo halikosei. Badala ya kubishana, hebu tumwinue Bwana, na tukabiriane na wapinzani kama vile Bwana alivyofanya, akitumia “Imeandikwa”. Hebu na tuinue bendera ambayo imeandikwa: “Biblia ndiyo kanuni ya imani yetu na nidhamu yetu”. —(Ellen G. White, Sellected Messages Vol. 1 (1SM), p. 416, par. 2); pia The Review and Herald December 15, 1885, Art. A par. 16)))

“Neno la Mungu halina budi kutambuliwa kama mamlaka iliyo juu ya mamlaka yote ya wanadamu. ‘Bwana asema hivi’ Haipaswi kuwekwa kando na badala yake kuweka kanisa limesema hivi, au serikali yasema hivi.” —(Ellen G. White, The Acts of the Apostles (AA), p. 68, par. 2); pia Christian Service, p. 161.3; Gospel Workers 1915, p. 389.2; God’s Amazing Grace, p. 59.5; To Be Like Jesus, p. 61.3; Conflict and Courage, p. 329.5; The Faith I Live By, p. 240.3; na My Life Today, p. 280.4)))


Umoja ni wa lazima miongoni mwa watu wa Mungu

“Umoja ni nguvu; utengano ni udhaifu. Wakati wale wanaoamini ukweli wa sasa wanapokuwa na umoja, wanakuwa na ushawishi wa kuonekana” —(Counsels for the Church (CCh), p. 291, par. 3); pia Testimonies for the Church, vol. 5, p. 236.2; Testimony Treasures, vol. 2, p. 77.2; na The Signs of the Times January 18, 1883 paragraph 2)))

“Kuungana na Kristo pamoja na sisi kwa sisi ni usalama wetu pekee, katika siku hizi za mwisho. Hebu tusifanye iwezekane kwa shetani kuwanyooshea kidole washiriki wa kanisa letu, na kusema; ‘Tazama jinsi watu hawa waliosimama chini ya bendera ya Kristo, wanavyochukiana wao kwa wao. Hatuna kuhofia kwa maana wanatumia nguvu nyingi kupigana wao kwa wao kuliko kupigana vita na jeshi langu.” —(Ellen G. White, Counsels for the Church (CCh), p. 43, par. 2); pia Testimonies for the Church, vol. 8, p. 240.2; The Upward Look, p. 358.2; Testimony Treasures, vol. 3, p. 244.2; The Southern Watchman February 2, 1904, Art. A paragraph 8; Manuscript 143, 1903, par. 5; na Manuscript 149, December 31, 1903 par. 8)))

“Kadri ambavyo tunaukaribia mgogoro wa mwisho, ni wakati wa muhimu kwamba mapatano na umoja viwepo miongoni mwa vifaa vya Bwana.” —(Ellen G. White, Testimonies for the Church, vol. 7, p. 182, par. 2); pia Testimony Treasures, vol. 3, p. 171.2; The Publishing Ministry, p. 114.4; Last Day Events, p. 131.5; na Maranatha, p. 187.2)))

Lakini hata hivyo, umoja ni katika kweli tu, na Roho, na si katika makosa

a. Hakuna umoja kati ya ukweli na makosa.

“Tunapaswa kuungana, lakini si kwenye jukwaa la makosa.” —(Ellen G. White, Manuscript Releases, vol. 15 (15MR), p. 259, par. 2); pia Special Testimonies, Series B02, p. 41.2; Battle Creek Letters, p. 111.5; Letter 281, 1904, par. 5; na Manuscript 76, 1904, par. 11)))

“Baadhi watachukua nadharia ambazo zitatafsiri vibaya Neno la Mungu, na kudhoofisha msingi wa kweli ambao umekwisha kuimarishwa, hatua kwa hatua, na kutiwa muhuri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Ukweli wa zamani unapaswa kuhuishwa ili kwamba nadharia za uongo ambazo zimekuwa zikiletwa na adui kwa busara ziweze kuzuiliwa. Hapawezi kuwa na umoja kati ya ukweli na kosa. Wale ambao wameongozwa katika udanganyifu tunaweza kuungana nao ikiwa tu wameachana na udanganyifu huo.” —(Ellen G. White, Letter 121, March 15, 1905, par. 10); pia The Upward Look, p. 88.2))

“Ukweli wa Mungu ni kati ambayo kwa hiyo uelewa unafikiwa. Roho Mtakatifu imetolewa kwa wakala wa kibinadamu ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na mawakala wa kiungu. Inageuza akili na tabia, ikimsaidia mtu kuvumilia kana kwamba anamwona Yeye ambaye haonekani. Upendo kamili unaweza kufurahiwa kupitia tu imani ya ukweli na upokeaji wa Roho Mtakatifu.” —(Ellen G. White, The Upward Look, p. 104.2)pia Our Father Cares, p. 261.2)))

“Baadhi ambao hujidai kuwa waaminifu kwa sheria ya Mungu wamejitenga na imani na wamewadharirisha watu Wake katika vumbi, wakiwawakilisha kuwa wamoja na watu wa kidunia. Mungu ameliona na kuliandika jambo hili. Wakati umefika ambao, kwa gharama yoyote, tunapaswa kuchukua msimamo ambao Mungu ametupa. Waadventista Wasabato wanapaswa sasa kusimama tofauti na tofauti, watu walioitwa na Bwana kama watu wake. Wasipofanya hivyo, Hawezi kutukuzwa ndani yao. Ukweli na uongo haviwezi kusimama katika ushirikiano. Hebu sasa tusimamie mahali ambapo Mungu amesema kwamba tunapaswa kusimamia. Hebu tufanye yote katika nguvu zetu kujiokoa wenyewe kutoka kwenye udhalilishaji wa kutisha ambao tumejiweka chini yake. Tunapaswa kujitahidi ili kupata umoja, lakini si kwa kiwango cha chini cha kuzingatia sera ya kidunia na kufanya muungano na makanisa maarufu.” —(Ellen G. White, Letter 113, May 1903, par. 6); pia Mind, Character, and Personality, vol. 2, p. 559.2)))

“Upendo kama wa Kristo huunganisha moyo kwa moyo. Ukweli huwavuta watu pamoja. Huwaleta kwenye maelewano na umoja wale wote ambao imani yao ni hai, yenye bidii katika Mwokozi. Kristo aliunda kwamba wale wanaomwamini waendelee na kuwa na nguvu kwa kuhusiana mmoja kwa mwingine. Wote ambao hufanya kazi bila ubinafsi katika kazi ya Bwana wamebeba ushahidi kwa ulimwengu kwamba Mungu alimtuma Mwana wake duniani.” —(Ellen G. White, The Upward Look p. 104.4); pia Our Father Cares, p. 261.4; na Manuscript 46, March 31, 1902, par. 6)))

“Ni mapenzi ya Mungu kwamba umoja na maelewano vinapaswa kuwepo miongoni mwa watu wake. Mwokozi wetu aliomba kwamba wanafunzi wake wawe na umoja kama Yeye alivyo umoja na Baba. Lengo letu siku zote linapaswa kuifikia hali hii ya umoja; lakini kwa kufanya hivi hatupaswi kutoa kafara kanuni moja ya ukweli. Ni kwa njia ya kuuti ukweli ndipo tunatakaswa; kwa maana wakati Yesu anaomba kwamba wafuasi wake wawe na umoja, aliomba pia, ‘Uwatakase katika kweli.'” —(Ellen G. White, The Signs of the Times May 12, 1881 paragraph 21)

“Kama imani yako katika neno la Mungu imeimarishwa; kama utakubali kikamilifu ukweli ambao umetuita sisi kutoka nje ya dunia na kutufanya sisi kuwa watu walioitwa na Bwana kama hazina yake ya pekee; kama utaungana na ndugu zako katika kusimama na alama ya mipaka ya zamani, ndipo umoja utakuwepo. Lakini unabaki katika kutoamini, haujatulia katika msingi wa kweli wa imani; hapawezi kuwa na tumaini la umoja zaidi katika wakati ujao kuliko ilivyokuwa wakati wa nyuma.” —(Ellen G. White, Manuscript Releases, vol. 11 (11MR), p. 319, par. 1); pia Letter 23, December 1903 par. 2; na Spalding and Magan Collection, p. 341.2)))

ZINAKUJA ZAIDI.

Comments are closed.

%d bloggers like this: