KUPITISHWA KWA FUNDISHO LA UTATU Mtakatifu mwaka wa 325.BK

Mjadala wa Kupitishwa Kwa fundisho la Utatu Mtakatifu ulianzishwa kwenye Mkutano uliofanyika katika mji wa Nikea, mwaka wa 325 Baada Ya Kristo (BK) Chini ya usimamizi wa Mfalme Constantino wa Roma na kuhudhuria
na Maaskofu wapatao 300 toka sehemu mbalimbali duniani.
Lengo la mkutano lilikuwa ni kujadili nafasi ya Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu
katika Mungu mmoja, jambo ambalo lilikuwa, Halijulikani Kwa Hapo Kabla.” 

Fundisho La Utatu Ni Kanuni Ya Imani Ya Nikea Na Wala Siyo Kanuni Ya Imani Ya Ukristo,

“Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni fomula rasmi ambayo ilipitishwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325)[1] ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381) ili kubainisha imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya uzushi, hasa wa Ario na wafuasi wake.

Katika mazingira hayo, lengo kuu lilikuwa kwanza kumkiri Yesu kama Mungu kweli sawa na Baba, halafu kwamba Roho Mtakatifu anastahili kuabudiwa pamoja na Baba na Mwana (Utatu Mtakatifu).
“kwahiyo Hadi leo hiyo kanuni ya imani Ya Nisea inatumika sana katika madhehebu mengi ya Ukristo”

Imani hiyo ilizidi kufafanuliwa hasa katika karne IV, mitaguso mikuu ya kwanza ilipochukua msimamo dhidi ya watu waliokua Wakipinga Fundisho La Utatu Ambalo Ndiyo Kanuni Kuu Ya Imani Ya, Nisea-konstantinopoli inayotumika hadi leo katika madhehebu mengi ya Ukristo.

Video ya Utatu katika Misiri


Historia Inaeleza Ya Kwamba Hata Chanzo Cha Ufalme Wa Papa Kuyaangusha Yale Mataifa Matatu Ni Kutokana Na kwamba wao hawakutaka Kuliamini Fundisho La Utatu”
Ufunuo 17:5 inasema, yule “mwanamke amekaa juu ya mnyama…mwenye pembe kumi“. Pembe katika unabii inawakilisha “mfalme/ufalme” au “taifa”, Danieli akitabiri kuhusu mnyama Roma alisema, “Na habari za zile pembe kumi [za mnyama], katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataoondoka baada ya hao;…naye atawashusha wafalme watatu” Danieli 7:24.
Hivyo pembe kumi ni wafalme kumi ambao wanatawala katika ufalme huo mmoja wa Roma. Baada ya dola la Roma kuanguka mwaka 476BK liligawanyika katika mataifa/wafalme kumi ambayo ni…

1    Saxon, kwa sasa ni taifa la Uingereza.
2    Frank, kwa sasa ni taifa la Ufaransa.
3    Alamanni, kwa sasa ni taifa la Ujerumani.
4    Visigoth, kwa sasa ni taifa la Uhispania.
5    Suevi, kwa sasa ni taifa la Ureno.
6    Lombard, kwa sasa ni taifa la Italia.
7    Burgundia, kwa sasa ni taifa la Uswidi.
8    Heruli, liling’olewa na pembe ndogo 493 B.K.
9    Vandal, liling’olewa na pembe ndogo 534 B.K.
10    Ostrogoth, liling’olewa na pembe ndogo 538 B.K.
Hizo ndio pembe kumi za mnyama Roma, Unabii katika Danieli 7:8 na 24 unasema kuwa, baada ya pembe hizo kumi ambazo ni wafalme kumi wa dola la Roma, kati yao ingetokea pembe nyingine ndogo ambayo ni mfalme mwingine, ambaye ni Upapa wa Vatikani; nao ungelikuwa tofauti na wale wafalme 10 kwa sababu una nguvu za kidini na kiserikali tofauti na wale 10. Pia pembe ndogo ambaye ni Upapa angezing’oa pembe 3 katika zile pembe 10 za mnyama Roma.

Baada ya kanisa katoliki kupitisha fundisho la utatu katika baraza la 2 huko Konstantinapoli mwaka 381bk, baraza liliamuru kwamba wote wasiokubaliana na imani ya utatu waangamizwe; hivyo mataifa ya Waario (Arians); watu ambao hawakuamini fundisho la utatu, mataifa yao matatu; Heluli, Vandalis, na Ostrogoth yaliangushwa na kanisa Katoliki. Hivyo Upapa ulizing’oa kabisa pembe hizo 3 kama Danieli alivyotabiri, na mataifa 7 yaliyobaki leo yanaitwa Umoja wa Ulaya [EU].

Wakatoliki Wao Hufundisha Hivii
“Fumbo la Utatu Mtakatifu ni kiini cha imani ya Kanisa. Katoloki- RV
Kwa Jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu Amina. Imani yetu imejengwa katika msingi huu: Tunaamini katika Mungu mmoja aliye katika nafsi tatu, yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kanisa linatufundisha kwamba mgawayiko huu wa nafsi hujidhihirisha katika kazi zao: Baba ndiye muumbaji, Mwana ni mkombozi na Roho Mtakatifu ni mfariji. Utangulizi wa Ekaristi wa Sherehe ya Utatu Mtakatifu unaelezea kwa kifupi imani hiyo ukisema: “Wewe (Baba) pamoja na Mwanao wa pekee na Roho Mtakatifu u Mungu mmoja na Bwana mmoja, siyo katika umoja wa nafsi, ila katika utatu wa Mungu mmoja”. Nafsi hizi tatu katika umungu mmoja zina utukufu ulio sawa na kamwe hazigawanyiki. Hii ndiyo imani yetu, Wakatoliki.

(*Radio Vatican Katika Mitandao Ya Kijamii*)


LAKINI FUNDISHO LA YESU KRISTO NA MITUME WAKE LINAFUNDISHA HIVI.

YESU.  Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Yohana 17:3

PETRO:  Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo……1 Petro 1:3

PAULO:  Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Waefeso 4:6

lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. 1 Wakor 8:6

Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. Wag 3:20

Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 1 Timotheo 2:5

YAKOBO: Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Yakobo 2:19

Swali kwako, Je! unaamini fundisho la Roman Catholiki (TRINITY ) Ama Fundisho la Yessu Kristo na Mitume. Wake?

Leave a comment